Why Nostr? What is Njump?
2024-06-09 06:39:16

Bitcoin safari community on Nostr: *Kuna Cha Kujifunza Hapa...!* Kondoo alikuwa anapita akamuona simba akilia akiwa ...

*Kuna Cha Kujifunza Hapa...!*

Kondoo alikuwa anapita akamuona simba akilia akiwa amenasa kwenye boksi la chuma(grili)...simba akamsihi sana kondoo amuokoe na kumuahidi kuwa hatamuua wala kumla, lakini kondoo akakataa.... Baada ya simba kubembeleza sana na kwa upumbavu wa kondoo, akafungua lile boksi la chuma.

Sasa simba alikuwa na njaa kali mno baada ya kukaa kifungoni kwa siku kadhaa bila kula chakula... Mara moja alimrukia kondoo na kukaribia kumuua ili amle, lakini kondoo alimkumbusha kiapo chake.

Waliendelea kubishana hadi wanyama wengine waliokuwa wanapita wakauliza kulikoni? Basi simba na kondoo wote wakaelezea jinsi ilivyokuwa, lakini kwa hofu ya simba na kutaka kupata huruma machoni pa simba, wanyama wote wakamsapoti simba isipokuwa kobe ambaye alidai kuwa hakuelewa mazingira na stori yenyewe.

Sasa kobe akamuomba simba aoneshe mahali alipokuwa kabla ya kondoo kumuokoa, simba akamuonesha kobe kwa mguu wake wa mbele, pale... Kobe akamuuliza tena, "ulikuwa ndani ama nje kabla ya kondoo kuja??"...Simba akamjibu, "nilikuwa ndani".

Kobe akamuuliza tena simba, "sawa, embu ingia tena ili tuone jinsi ilivyokuwia vigumu kukaa ndani ya grili kwani sielewi stori hii yote vizuri"... Simba akaingia, na mara moja(chapu!), kobe akafunga lile boksi la chuma (grili)... Na simba sasa alikuwa amenasa tena!!_

Kwa mshangao mkubwa, wale wanyama wengine wakamuuliza kobe "Kwanini?" na kobe akawajibu..."Kama tukimruhusu simba amle kondoo leo, bado atasikia njaa tena kesho na hatujui kati yetu ni nani atakayeliwa kesho..!!"

HADITHI HII INATUFUNDISHA NINI?

Usiunge uovu mkono leo kwa vile haukuathiri moja kwa moja, kesho inaweza kuwa zamu yako.!!

tunahitaji kobe wengi zaidi katika jamii yetu.

Mi nimetaja tu wanyama hapa mjue hilo🤣🤣🤣
Author Public Key
npub1t8cxvze5m4y0nhavtktnkamhff667pt75w3xzg22chxue4wjg3qqufsqc6